Home Uncategorized JONAS MKUDE AWAPOTEZA WOTE NDANI YA SIMBA

JONAS MKUDE AWAPOTEZA WOTE NDANI YA SIMBA


 KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mzawa anayelipwa mshahara mkubwa Bongo.

 

Wakati yeye akiongoza kwa wachezaji wazawa, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone raia wa Msumbiji ndiye anayeongoza kukunja mshahara mkubwa kwa wachezaji wageni ambaye yeye anachukua dola 7,000 (zaidi ya Sh 16m) kwa kila mwezi.

 

Inadaiwa kuwa Mkude anakunja Sh 8m kila mwezi tangu alipoongezwa mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu wa 2018/19.


Mkude alipewa mkataba huo baada ya kuwepo tetesi za nyota huyo kuwaniwa na Yanga katika msimu wa 2018 ambapo mkataba wake ulikuwa umemalizika kuendelea kubaki Simba.


Kiungo huyo mwenye uwezo wa kukaba na kupiga pasi fupi na ndefu Desemba 28 alisimamishwa kazi kwa kile kilichotajwa utovu wa nidhamu huku sababu ya kusimamishwa ikifichwa.

 

Cheki ‘Top Five’ ya wachezaji wazawa wanaolipwa mishahara mikubwa katika Ligi Kuu Bara baada ya Mkude kuongoza ambao ni:-


FARID MUSSA.

 

Kiungo mshambuliaji wa Yanga ndiye anayefuatia kwa kuwa inadaiwa anakunja Sh 7m kwa mwezi tangu alipojiunga na timu hiyo katika msimu huu akitokea Tenerife FC ya Hispania.

 

JOHN BOCCO


Nahodha na mshambuliaji wa Simba anashika nafasi ya tatu kwa kulipwa Sh 7m na analipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kuongeza mkataba katika msimu wa 2018.

 

Bocco alipewa mkataba huo baada ya kuelezwa kuwa Azam FC walikuwa na mipango ya kumrejesha klabuni hapo.


ERSATO NYONI


Beki na kiungo wa Simba ambaye inadaiwa kuwa analipwa Sh 7m kila mwezi, dili ambalo alisaini mwaka 2018.

 

AISHI MANULA


Kipa namba moja wa Simba naye analipwa Sh 7m kila mwezi, naye dili lake la mwisho la mkataba alisaini mwaka 2018.Manula anapewa changamoto uwanjani na Beno Kakolanya lakini bado Manula ameendelea kuwa chaguo la kwanza kikosini hapo.

SOMA NA HII  AZAM FC YAKUBALI MAMBO NI MAGUMU NDANI YA LIGI