Uncategorized

BEKI HUYU MZAWA AINGIA ANGA ZA YANGA

admin January 10, 2021 12:47 pm


 DICKSON Job beki chipukizi ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Turiani, Morogoro anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga.

Habari zimeeleza kuwa mabosi wa Yanga chini ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa timu hiyo wanahitaji kufunga na usajili wa nyota wawili ambapo mzawa ni mmoja na mgeni ni mmoja.

Kwa upande wa wageni anatajwa kuwa atakuwa mshambuliaji huku kwa wazawa akitajwa Job kuwa yupo kwenye hesabu za kuibukia ndani ya Yanga.

Mtu wa karibu wa Job amesema kuwa nyota huyo amekuwa ni mwenye furaha kwa wakati huu kila anapozungumza naye kuhusu ishu yake ya kwenda Yanga.

“Job kwa sasa yupo kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, ila amekuwa akionekana mwenye furaha kila nipozungumza naye kuhusu kwenda Yanga hivyo nadhani kuna jambo anaficha,” alisema.

Kwa upande wa Job mwenyewe amesema kuwa ikiwa kuna timu inahitaji saini yake ni suala la kufuata utaratibu.

NI SIMBA V NAMUNGO NUSU FAINALI, YANGA YAMSUBIRI MSHINDI WA LEO VIDEO:HUYU NDIYE KOCHA WA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply