Home Uncategorized GWAMBINA YAPOTEZA POINTI TATU MBELE YA BIASHARA UNITED

GWAMBINA YAPOTEZA POINTI TATU MBELE YA BIASHARA UNITED


 KIKOSI cha Biashara United chenye maskani yake Mara leo Januari 3 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina FC.


Ikiwa Uwanja wa Gwambina Complex imeibuka na ushindi huo kwa bao la Deogratius Mafie aliyepachika bao hilo dakika ya 15.

Jitihada za wachezaji wa Gwambina FC kuweka mzani sawa ziligonga mwamba kwa kuwa kipindi cha pili hakuna timu iliyoweza kupata bao.

Rekodi zinaonyesha kwamba Gwambina FC leo ikiwa nyumbani imepiga mashuti 9 huku Biashara United ikipiga jumla ya mashuti nane.

Kwa Gwambina ni mashuti mawili yalilenga lango na mashuti saba hayakulenga lango huku mashuti matatu kwa Biashara United yalilenga lango na mashuti matano hayakulenga lango.


Leo umekuwa ni mchezo wa kwanza kwa nyota mpya wa Gwambina, Mrisho Ngassa kuanza kuitumikia timu yake mpya baada ya kusaini dili jipya kwenye dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16,2020 linatarajiwa kufungwa Januari 15.

SOMA NA HII  BARCELONA YACHAPWA 3-1 NA REAL MADRID, ANSU ATUPIA