Home Yanga SC HII HAPA KUFURU YA YANGA KWA JEMBE LAO JIPYA

HII HAPA KUFURU YA YANGA KWA JEMBE LAO JIPYA


 

UNAAMBIWA usiulize kuhusu mshahara wa mshambuliaji mpya wa Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak, kwani walichokifanya Yanga kwa mshambuliaji huyo ni kufuru.

Taarifa za ndani ya Yanga zinaeleza kuwa straika huyo amepewa mkataba utakaomfanya alipwe kiasi cha dola za Kimarekani 9500 sawa na fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 22 kwa mwezi.

Tayari Yanga imeshatangaza kumsajili Fiston ambaye ni raia wa Burundi aliyekuwa akiitumikia Klabu ya Enppi ya nchini Misri.

Mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema: “Taarifa sahihi juu ya usajili wa Fiston mimi najua wazi kuwa hadi tunamalizana naye tulikubaliana kumlipa mshahara wa dola 9500, kwa kila mwezi,”

SOMA NA HII  LUC EYMAEL 'AWARUDI' YANGA KIVINGINE