Home Uncategorized MSHAMBULIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA AIBUKIA POLISI TANZANIA

MSHAMBULIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA AIBUKIA POLISI TANZANIA


MSHAMBULIAJI Gerald Mathias Mdamu, ambaye alikuwa ameingia kwenye rada za Klabu ya Yanga amesema kuwa ameamua kuibukia ndani ya Polisi Tanzania ili kupata changamoto mpya.


Nyota huyo mwenye pasi mbili za mabao ndani ya Biashara United awali ilitajwa kuwa yupo kwenye hesabu za mabosi wa jangwani, Yanga ambao walikuwa wanahitaji saini yake.

Yanga walikuwa kwenye hesabu za kuipata saini ya Mdamu pia msimu uliopita wakati ule alipokuwa akicheza ndani ya Mwadui FC ila dili lake lilikwama na nafasi yake ikachukuliwa na Wazir Junior aliyekuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mbao.


Msimu huu wa 2020/21 alianza maisha yake ndani ya Klabu ya Biashara United chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza ila kwa sasa atakuwa ndani ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini akiwa amesaini dili la mwaka mmoja.

Mdamu amesema kuwa anahitaji kupata changamoto mpya na atazidi kupambana muda wote ili kuwa bora.


SOMA NA HII  UJUMBE WA RUVU SHOOTING HUU HAPA