Home Uncategorized NYOTA KMC ASIMAMISHWA KISA NIDHAMU

NYOTA KMC ASIMAMISHWA KISA NIDHAMU


UONGOZI wa 
Klabu ya KMC FC umemsimamisha mshambuliaji wa kikosi hicho Relliants Lusajo aliyeibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Namungo. 


Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa KMC,Christian Mwagala imeeleza namna hii:”Tunapenda kuwajulisha mashabiki na wapenzi wa Klabu ya KMC FC kuwa mchezaji Realint Lusajo amesimamishwa kutokana na sababu ya utovu wa nidhamu.


“Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni baada ya uongozi kujiridhisha na kwamba mchezaji yoyote anapofanya makosa ya utovu wa nidhamu kwenye Timu atapaswa kupata adhabu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa.


“Wakati huo huo,uongozi wa KMC FC pia umetoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wake na kwamba watapaswa kurejea kambini Januari 15 mwaka huu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michezo ya Ligi kuu Soka ,”Tanzania Bara ambapo mchezo unaofuata KMC FC watakuwa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons.


SOMA NA HII  VIDEO: NYONI AWATULIZA MASHABIKI,SARE YA RUVU SHOOTING HAIJAWAPOTEZA HESABU