Home Simba SC NYOTA SIMBA QUEENS AWEKA REKODI YAKE BONGO

NYOTA SIMBA QUEENS AWEKA REKODI YAKE BONGO

 OPPAH Clement mshambuliaji wa kikosi cha Simba Queens amekuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga mabao saba ndani ya Ligi ya Wanawake msimu wa 2020/21.

Mshambuliaji huyo mwenye dred kichwani ni miongoni mwa washambuliaji wanaofanya vizuri ndani ya ardhi ya Bongo kwa sasa.

Alitupia mabao hayo wakati timu yake ya Simba Queens ikiibuka na ushindi wa mabao 11-1 dhidi ya Baobab Queens, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mo Simba Arena. 

Ilikuwa  Januari 25  wakati mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi ya Wanawake Tanzania wakisepa na pointi tatu muhimu.

Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kuwa nafasi ya pili na pointi zake ni 29 baada ya kucheza mechi 11 huku kinara akiwa ni Yanga Princess mwenye pointi 31.

Jumla mshambuliaji huyo mzawa anafikisha jumla ya mabao 20 kibindoni.

Nyota huyo amesema:”Malengo makubwa ni kuona timu inapata matokeo, ushindi ni furaha kwetu pamoja na mashabiki tunahitaji sapoti,” .

SOMA NA HII  KUHUSU USAJILI WA SIMU HUU....KIUNGO YANGA AICHOMOLEA SIMBA ...AFUNGUKA A-Z JINSI PESA INAVYOTUMIKA JANGWANI...