Home Uncategorized YANGA KUSHUSHA MASHINE YA KAZI, UONGOZI WAWEKA WAZI

YANGA KUSHUSHA MASHINE YA KAZI, UONGOZI WAWEKA WAZI


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo kwenye mpango wa kukamilisha usajili wa mshambuliaji mmoja ambaye atakuja kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho akisaidiana na nyota wengine waliopo ndani ya kikosi hicho.


Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa imecheza mechi 18 bila kupoteza kwa msimu wa 2020/21 ikiwa imekusanya pointi 44.

Mchezo wake wa mwisho ndani ya 2020 ilimaliza kwa kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa mipango ipo wazi na watamtambulisha nyota huyo hivi karibuni.

“Kila kitu kuhusu usajili wa mchezaji wetu mpya upo tayari na atakuja kuongeza nguvu kikosini, kikubwa mashabiki wasiwe na mashaka tutafanya vizuri.

“Hatuwezi kumuweka wazi kwa sasa kwa sababu ni makosa ambayo tumewahi kuyafanya siku za nyuma wachezaji wetu wakapata matatizo, kilichopo kwa sasa ni kuona kwamba wachezaji wanakuja baada ya kukamilisha utaratibu,” amesema.


Jembe ambalo linatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga ni Ferebory Dore raia wa Congo ambaye amecheza soka la kulipwa kwa mafanikio nchini Ufaransa.

SOMA NA HII  YANGA WAMCHUNIA BOBAN, MENEJA WAKE AFUNGUKA