Home Uncategorized YANGA KUTUMIA KOMBE LA MAPINDUZI KUSAKA MEJEMBE YA KAZI

YANGA KUTUMIA KOMBE LA MAPINDUZI KUSAKA MEJEMBE YA KAZI


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa utatumia mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambalo linaendelea kumpata nyota mmoja ambaye ataingia moja kwa moja kwenye kikosi hicho.

Miongoni mwa nyota ambao wanatazamwa kwa ukaribu ni pamoja na nyota wa Klabu ya Chipukizi Fakh Sharif aliyemtungua kipa namba mbili Beno Kakolanya kwa shuti kali akiwa chini ya uangalizi wa mabeki wa Simba ambao hawakuwa na chaguo.

Mbali na nyota huyo pia inaelezwa kwamba kuna kiungo mwingine ambaye anacheza ndani ya Mlandege FC iliyocheza na Azam FC mchezo wa ufunguzi wakitoshana sare ya kufungana bao 1-1 huku mfungaji kwa Azam FC akiwa ni Mpianza Monzinzi na lile la Mlandege likifungwa na Rashid Mandawa.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa nguvu kubwa kwa sasa ipo kwenye Kombe la Mapinduzi na ikitokea wakampata mchezaji mzuri watampa mkataba.

“Dirisha la usajili bado linaendelea na ikitokea akapatikana mchezaji huku anaweza kusajiliwa kwani hakuna timu isiyopenda kuwa na mchezaji mzuri.


“Kwenye Kombe la Mapinduzi tuna jambo letu ambalo tunahitaji kufanya ni suala la kusubiri, kikubwa ambacho tutakitazama ni ripoti ya mwalimu” .


Kwa sasa Yanga inapambana kusaka mshambuliaji ambaye ataibuka ndani ya kikosi hicho kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Michael Sarpng mwenye mabao manne sawa na Yacouba Songne.

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi saa 10:15 jioni.


Simba pia itakuwa uwanjani saa 8:15 hatua ya nusu fainali dhidi ya Namungo FC.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTWAA KOMBE, HAZARD KUSEPA CHELSEA