Home Uncategorized YANGA YAIVUTIA KASI NAMUNGO

YANGA YAIVUTIA KASI NAMUNGO

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Namungo FC. 


Yanga ilifungua pazia Januari 6 kwa kucheza na Klabu ya Jamhuri ambapo dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu.


Mchezo huo ulichezwa saa 8:15 usiku hivyo kesho itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Klabu ya Namungo.


Kaze amesema:”mchezo wa Kwanza tulikutana na timu nzuri ambayo ilikuwa inapambana ndani ya uwanja tutaingia kwenye mchezo wa pili kwa tahadhari tukisaka ushindi,” .


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Amaan, saa 8:15 usiku, bingwa mtetezi wa taji hilo ni Mtibwa Sugar ambaye alitwaa msimu wa 2020 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.

SOMA NA HII  MCHUNGAJI MASHIMO, MANARA HAPATOSHI!