STAA wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ametolewa kwenye kikosi cha Yanga kitakachomenyana na Kengold FC kwenye mchezo wa michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kutokana na matatizo ya kifamilia.
Yanga inatarajia kucheza mchezo huo wa ASFC, kesho Jumamosi dhidi ya Kengold FC kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.
Mchezo wa mwisho kucheza Ntibazonkiza ulikuwa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC ambapo alifunga bao moja.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka Klabu ya Yanga, kimeeleza kuwa mchezaji huyo alipona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.
“Saido alipona majeraha yake lakini kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar aliaga kuwa ana matatizo ya kifamilia hivyo anaenda kwao Burundi.“Aliondoka Jumamosi lakini mpaka leo hajaonekana na hajarejea kikosini hivyo tutamkosa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Daktari ya Yanga, Nahum Muganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana muda mrefu tangu aanze majukumu yake klabuni hapo. Alipotafutwa Ofisa Mhamasishaji, Antonio Nugas hakupatikana hadi gazeti linaingia mtamboni.
STORI: MUSA MATEJA, Dar es Salaam
nd_user – Nice Article! SAIDO APONA, ATIMKIA BURUNDI