Home Simba SC KAGERE AANDIKA HISTORIA MBELE YA AZAM

KAGERE AANDIKA HISTORIA MBELE YA AZAM


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Simba, Meddie Kagere ameandika historia mbele ya klabu ya Azam baada ya kufanikiwa kuifu

nga timu hiyo katika michezo mitatu mfululizo ‘back to back’ aliyokutana nao kwenye Ligi Kuu Bara.

Kagere Jumapili iliyopita aliifungia Simba bao la kuongoza katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam, mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.

Msimu uliopita katika mchezo wa raundi ya kwanza, Kagere alifanikiwa kuifungia Simba bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 walioupata Simba Januari 10, na kufanya hivyo tena katika mchezo wa raundi ya pili ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 Machi 4, mwaka jana.

Bao alilofunga Kagere katika mchezo wa Jumapili  limemfanya kufikisha mabao tisa na kumpiku nahodha wake John Bocco mwenye mabao nane, hivyo kuongoza chati ya wafungaji msimu huu.

SOMA NA HII  DIRISHA DOGO ....SIMBA KUBEBA VIFAA HIVI KUTOKA ANGOLA...MGUNDA AWAPITISHA ...