Home kimataifa KOCHA SPURS ANATAJWA KUWEKWA KWENYE HESABU ZA KUFUTWA, ATOA KAULI YA KISHUJAA

KOCHA SPURS ANATAJWA KUWEKWA KWENYE HESABU ZA KUFUTWA, ATOA KAULI YA KISHUJAA


 JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Spurs amesema kuwa licha ya mambo kuwa magumu ndani ya kikosi hicho bado hajakata tamaa.

Mreno huyo amesema kuwa wataendelea kupambana ndani ya uwanja ili kupata matokeo chanya ambayo yatawafanya warejee kwenye ubora wao wa awali.

Kwa sasa Mourinho amekuwa kwenye presha kubwa na inaaminika kwamba huenda akafutwa kazi kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri.

“Ni ngumu lakini bado inawezekana kwetu kurejea kwenye ubora wetu na kufanya mambo yaweze kwenda sawa ndani ya uwanja.

“Licha ya kwamba Ligi Kuu England ni ngumu na kimahesabu inawezekana kuwa katika hali ya awali ndani ya uwanja,”.

Spurs ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo na ina pointi 36 baada ya kucheza mechi 23.

SOMA NA HII  CITY YAPOTEZA MBELE YA TOTTENHAM