Home Simba SC LUIS, WAWA WAREJEA KIKOSI CHA SIMBA TAYARI KUIVAA DODOMA JIJI

LUIS, WAWA WAREJEA KIKOSI CHA SIMBA TAYARI KUIVAA DODOMA JIJI


 NYOTA wawili wa kikosi cha Simba ambao walikosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC Luis Miquissone na  Pascal Wawa wanatarajiwa kuanza leo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.

Nyota hao wawili pamoja na kiungo mkabaji Taddeo Lwnga walikuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kwa upande wa Lwanga yeye atakosekana kwenye mchezo wa leo kwa sababu amepata matatizo ya kifamilia mpaka pale atakapokamilisha masuala hayo atarejea.

Akizungumza na Saleh Jembe, Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa Luis na Pascal tayari wamereja baada ya kumaliza adhabu za kutumikia kadi tatu za njano.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji wachezaji wetu wawili ambao ni Luis na Pascal watarejea kwa sababu adhabu ya kadi tatu za njano imeisha.

“Ni Lwanga atakosekana kwani bado ana matatizo ya kifamilia baada ya kupata msiba wa dada yake, maandalizi pamoja na mipango mingine inakwenda sawa,” .

Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku, mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri Dodoma ubao ulisoma Dodoma Jiji 1-2 Simba.

SOMA NA HII  SAKHO NAYE ANYOOSHA MIKONO SIMBA...WAKALA WAKE AGUNGUKA A-Z...AZAM FC WAHUSISHWA..