Home Ligi Kuu MTIBWA SUGAR YATAJA SABABU YA KUPIGWA 5G

MTIBWA SUGAR YATAJA SABABU YA KUPIGWA 5G

 


SOUD Slim, Kocha wa Makipa wa Mtibwa Sugar amesema kuwa walikutana na timu bora jambo ambalo likawafanya wafungwe mabao mengi.


Jana Aprili 14 Mtibwa Sugar ilikubali kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kichapo hicho kinawafanya Mtibwa Sugar kubaki nafasi ya 15 na mabao yao ya kufunga ni 9 wakiwa na pointi 24.

Slim amesema kuwa hawakuwa na namna ya kuwazuia wachezaji wa Simba kwa sababu walikuwa bora.

“Hakukuwa na namna ya kuwazuia wapinzani wetu kwa sababu walikuwa bora na tumefungwa na timu imara ambayo imetoka kucheza mechi za kimataifa.
“Makosa ambayo tumeyafanya tutayafanyia kazi kwa ajili ya mechi zijazo ili kupata matokeo chanya kwani wachezaji wetu bado wanaimarika,” .

Kwa kusepa na pointi tatu, Simba inafikisha jumla ya pointi 49 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi imecheza mechi 21.
SOMA NA HII  JKT TANZANIA YAIPIGA MKWARA SIMBA