MTASHANGAA na hamtaamini! Ndiyo maneno ambayo yatatumika leo pale Simba itakapokuwa ikiingia uwanjani kuwavaa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Leo majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, Simba itashuka uwanjani mbele ya mashabiki zaidi ya 10,000 kuisaka rekodi ya kupindua meza kwa kupata ushindi wa tofauti ya mabao 5-0 dhidi ya Kaizer, ili kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jumamosi iliyopita wakicheza ugenini katika Uwanja wa FNB (Soccer City), mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano hiyo, Simba walikumbana na kipigo cha mabao 4-0 ambayo yameweka rehani nafasi yao ya kutinga nusu fainali.
Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ameweka wazi kuwa wataingia katika mchezo wa leo dhidi ya Kaizer Chiefs siyo tu kusaka matokeo ya kufuzu hatua ya nusu fainali, bali wanakwenda kupambana kusaka heshima ya Klabu ya Simba na Watanzania.
Gomes alisema: “Tunahitaji kuwa bora hewani, lakini tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunamlinda yule mshambuliaji wao, Samir Nurkovic kwa kuwa ni straika mzuri na mwenye nguvu sana, hivyo ni lazima tutakapokutana tupambane naye kwa nguvu ili kumzuia.
“Tunatakiwa kupambana kufa na kuwa hai ili kupata ushindi, wapinzani wetu wana faida ya mabao ambayo wameyapata hivyo tunakwenda kulipa kisasi,” .