Home Ligi Kuu BINGWA LIGI KUU MSIMU UJAO WA 2021/2022 KUPATA TSH MILIONI 500

BINGWA LIGI KUU MSIMU UJAO WA 2021/2022 KUPATA TSH MILIONI 500

 


Azam Media imebainisha kutoa bonusi ya Sh 500 milioni kwa misimu mitatu mfululizo kwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao wa 2021/2022.

Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema kwenye kila nafasi ya msimamo wa Ligi kutakuwa na bonusi kwa misimu mitatu ijayo.

“Bingwa atapata Sh 500 milioni, wa pili Sh250 milioni, watatu Sh225 milioni, wa nne Sh 200 milioni.

“Kila nafasi kutakuwa na bonusi yake hadi mwisho, timu zote za Ligi mwishoni mwa msimu itapata chochote.

Alisema itakayomaliza ya tano itapata Sh 65 milioni, 60 milioni timu itakayomaliza ya sita na ya saba itapata 55 milioni,  na bonusi hiyo itaendelea kushuka hadi kwenye timu itakayocheza Playoff ambayo itapata bonusi ya Sh 20 milioni

“Bonusi itaongezeka kila msimu katika kipindi cha miaka 10, lengo ni kuhakikisha klabu zinasafiri vizuri, zinalipa wachezaji wake na kuweza kusafiri,”

SOMA NA HII  MBINU ZA KOCHA WA KAGERA SUGAR ZAFELI KWA TIMU YAKE YA ZAMANI