Home Simba SC DUH! KUMBE SIMBA WANATAKA YANGA ISHUSHWE MADARAJA MAWILI

DUH! KUMBE SIMBA WANATAKA YANGA ISHUSHWE MADARAJA MAWILI

 


KUFUATIA kuahirishwa kwa mchezo kati ya 
Simba na Yanga uliotakiwa ufanyike juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, hatimaye uongozi wa Simba umetoa tamko rasmi ukizitaka mamlaka ziwashushe madaraja mawili Yanga.

Taarifa za jana Jumapili kutoka katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba, ilisema:-“Sote tunajua kitendo kilichofanywa na Yanga tafsiri yake ni kwamba wamegomea mchezo na adhabu yake ni kushushwa madraja mawili na Simba kunufaika kwa kupewa alama tatu na mabao mawili.

“Mbali na hayo, pia kitendo chao ni sawa na usaliti kwa nchi na Serikali ambayo ilitoa maelekezo maalumu kusogezwa mechi kwa saa mbili zaidi.

“Hivyo basi kwa upande wetu tunaamini ahirisho lile la mechi limefanywa makusudi na Bodi ya Ligi kwa nia ya kuipendelea Yanga ambayo ilipaswa itii maagizo yao na ya TFF juu ya muda wa kuanza kwa mechi kama ilivyoelekezwa na Serikali na kisha kutujulisha sisi.

“Simba imesikitishwa sana na uamuzi huo wa Bodi ya Ligi ambao unaonyesha dhamira ovu juu ya klabu yetu na jambo jingine linaongeza mashaka juu ya kadhia hii ni kuiruhusu Yanga kuingia uwanjani kinyume na utaratibu wa muda maalumu unaoruhusiwa kabla ya kuanza kwa mchezo husika.”


SOMA NA HII  BAADA YA KUHISI PENGINE SIMBA WANAWEZA KUMUACHA KWELI...MORRISON AWAHI NA KUFICHUA HAYA...