Home epl KIPA WA LIVERPOOL AONGEZEA KASI VITA YA NNE BORA LIGI KUU ENGLAND

KIPA WA LIVERPOOL AONGEZEA KASI VITA YA NNE BORA LIGI KUU ENGLAND


KIPA wa Klabu ya Liverpool, Allison Becker amefufua matumaini ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Jurgen Kloop kuweza kumaliza ndani ya nne bora katika Ligi Kuu England.

Becker aliushangaza ulimwengu kwa kufunga bao pekee la ushinda dakika za lala salama na kuipa pointi tatu muhimu timu yake.

Ni Hai Robinson Kanu alianza kufunga kwa Westham United dakika ya 15 likawekwa usawa na mshambuliaji Mohamed Salah dakika ya 33.

Ngoma ilikuwa nzito Uwanja wa The Hawthorns mpaka muda wa dakika 90+5 ambapo kipa huyo alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya Liverpool kupata kona na kufanya ubao kusoma Westham United 1-2 Liverpool.

Sasa Klopp anahitaji pointi tatu katika kila mechi baada ya kucheza mechi 36 na kibindoni wana pointi 63 ikiwa nafasi ya kuweza kumaliza ndani ya nne bora ili ipate nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mkononi wana mechi mbili za kucheza ili kumaliza msimu huu wa 2020/21 wakiwa wameliacha taji lao likisepa na Manchester City ambao nao pia wamebakiwa na mechi mbili na mechi zote Liverpool itacheza wiki hii. 

Vita yao sasa ndani ya nafasi ya tatu na ya nne ni dhidi ya Leicester City iliyo nafasi ya tatu na ina pointi 66 pamoja na Chelsea iliyo nafasi ya nne na pointi 64 zote zimebakiwa na mechi mbili mkononi.

Mechi za Leicester City ni dhidi ya Chelsea, Mei 18 itakuwa ugenini na Tottenham itakuwa Mei 23 ambapo itakuwa nyumbani.

Chelsea wao ni dhidi ya Leicester City, Mei 18 itakuwa nyumbani na Aston Villa, Mei 23 itakuwa ugenini.

Kwa upande wa Liverpool wao wana mchezo dhidi ya Burnley itakuwa ni Mei 19 na ule wa mwisho ni dhidi ya Crystal Palace, Mei 23 itakuwa nyumbani.

SOMA NA HII  JUVENTUS YASANDA KWA LOCATELLI