Home epl LEO LIGI KUU ENGLAND NI MANCHESTER UNITED V LIVERPOOL

LEO LIGI KUU ENGLAND NI MANCHESTER UNITED V LIVERPOOL


 UWANJA wa Old Trafford leo kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Manchester United v Liverpool. 


Liverpool chini ya Jurgen Klopp haijawa na mwendo mzuri na haina uhakika wa kumaliza ndani ya nne bora.


Manchester United mambo yao yamekuwa tofauti kasi yao imekuwa ya moto kwani Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 33 na Liverpool ipo nafasi ya 6 ins pointi 54 nayo imecheza mechi 33.


Kinara ni Manchester City ambaye anapewa nafasi kubwa ya kusepa na taji hilo kibindoni ina pointi 80 imecheza mechi 34.


Rekodi zinaonyesha kwamba timu hizo mbili zimekutana mara 206, Manchester United imeshinda mechi 81 na Liverpool imeshinda mechi 67 na sare ni 58.

Kwa upande wa vinara wa kucheka na nyavu, Liverpool ni Mohamed Salah mwenye mabao 20 na pasi tatu za mabao huku Manchester United wao kinara wao ni Bruno Fernandes mwenye mabao 16 na pasi 11.

SOMA NA HII  JOSE MOURINHO:KUKASIRIKA KWA WACHEZAJI KAWAIDA WAKIFUNGWA