Home epl MANCHESTER UNITED IMERIPOTIWA WANAHITAJI SAINI YA KANE

MANCHESTER UNITED IMERIPOTIWA WANAHITAJI SAINI YA KANE

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Manchester United wanapiga hesabu za kuinasa saini ya nyota wa Tottenham, Harry Kane kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho msimu ujao.

Ripoti zimeeleza kuwa United wana matumaini makubwa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kucheka na nyavu.

Dau ambalo limewekwa mezani ili kumpata kwa ajili ya kujiunga na United kwa Kane ni euro milioni 90.

Mpango huo ulikuwepo kwa muda mrefu ila huenda ukakamilishwa kwa haraka kutokana na presha ambayo wanaipata kutoka kwa mashabiki ambao waliandama Jumapili ndani ya Uwanja wa Old Trafford jambo lililofanya mchezo wa United dhidi ya Liverpool upelekwe mbele.

Mashabiki wa United wamekuwa wakieleza kuwa hawana imani na Joel na Avram Glazer kutokana na uongozi wao kutokuwa na uwazi pamoja na kushindwa kupata mataji, jambo linalosababisha hasara kwao pamoja na suala la wao kujiunga na  European Super League kwa kuwa imesababisha hasara kwao.

SOMA NA HII  ULE MSIMU WA SOKA LA KIBABE UNAZIDI KUCHANJA MBUGA...HII HAPA LA LIGA NDANI YA DStv ...UTELEZI NI ULE ULE ....