Home Yanga SC MORO – NABI HAKUTAKA KUNISIKILIZA NA MIMI SIPENDI KUGOMBEZWA

MORO – NABI HAKUTAKA KUNISIKILIZA NA MIMI SIPENDI KUGOMBEZWA

 


BAADA ya sintofahamu juu ya Moro kutimuliwa kambini wakiwa Ruangwa mkoani Lindi kabla ya kucheza na Namungo, mwenyewe alifunguka na kuweka wazi kilichotokea mpaka kurejea Dar es Salaam.

Gazeti la  Mwanaspoti lilimtafuta kwa njia ya simu na kufanikiwa kuongea naye kwa kina na kueleza kilichotokea mpaka kuondoka kambini, ambapo alisema taarifa za utovu wa nidhamu anazoshutumiwa nazo sio za kweli kwa kuwa yeye ni majeruhi na alitumia nafasi hiyo kumuomba ruhusa Nabi, lakini hakutaka kumsikiliza.

Alisema Nabi anafahamu suala hilo na alimjulisha kabla ya kwenda Ruangwa, lakini hakutaka kumpa nafasi ya kumsikiliza na hata alipomuomba ruhusa ya kurejea kumuona daktari wake alishindwa kumwelewa.

“Mimi nilitumia taratibu, nikamfuata kocha nikamwambia kwa mara nyingine tatizo langu lililokuwa linanisibu, lakini mapokeo yake hayakuwa mazuri na mimi kama mtu mzima sipendi kabisa kugombezwa bila ya kusikilizwa,” alisema Moro.

“Ni sawa na baba ndani ya familia awe na mtoto, halafu anashindwa kusikiliza mahitaji yake.”

SOMA NA HII  YANGA IMLIPE TAMBWE MAPEMA HALAFU TUHAMIE HUKU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here