KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Juni 5 kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni lengo la kujiweka sawa kwa vikosi hivi vyote viwili vinavyoshiriki Ligi Kuu Bara.
Kwenye msimamo, Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina pointi 60 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.
Coastal Union ipo nafasi ya 16 ikiwa imekusanya pointi 33 baada ya kucheza mechi 30.