KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Farid Mussa, Alhamisi alikumbwa na gonjwa la hatari katikati ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
Farid ambaye katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar alianza kikosi cha kwanza, lakini ghafla akashindwa kuendelea kipindi cha pili.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Ruvu Shoting 2-3 Yanga.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Farid alisema, alishindwa kuendelea kipindi cha pili baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kutokwa vipele ghafla mwili mzima hivyo akalazimika kukimbizwa hospitalini kupatiwa matibabu.
“Baada ya kipindi cha kwanza kuisha tuliporudi vyumbani nikatokwa na vipele vingi mwili mzima.
“Nilipopelekwa hospitalini wakasema ni aleji na nimepewa dawa za kutuliza na hivi sasa nimeruhusiwa kurudi nyumbani, nimepewa dawa za kutumia na mpaka sasa naendelea vizuri,” alisema Farid.