Home Simba SC JOHN BOCCO ANALIAMSHA DUDE KILA BAADA YA DAKIKA 56

JOHN BOCCO ANALIAMSHA DUDE KILA BAADA YA DAKIKA 56


NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa bado watazidi kupambana ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea ndani ya Bongo ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

Bocco aliliambia Championi Jumatano kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa ila wao watapambana kufikia malengo yao.

 Wakati nahodha huyo mzawa akibainisha hayo rekodi zinaonyesha kuwa analiamsha dude uwanjani kila baada ya dakika 56.

Amecheza jumla ya mechi 16 kati ya 26 alikosekana katika mechi 10 ambazo timu hiyo imecheza.Nyota huyo amekuwa na ngekewa ya kufunga mabao muhimu ambayo yamekuwa yakiipa pointi tatu timu yake akiwa amehusika katika mabao 14 kati ya 61 ambayo yamefungwa na vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 64.

Wakati ubao wa Sokoine ukisoma Mbeya City 0-1 Simba na ule wa Kambarage uliposoma Mwadui 0-1 Simba ni yeye Bocco alitupia mabao hayo muhimu.

Kwenye mechi hizo 16 ametumia dakika 837. Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 56 jambo ambalo linazidi kukuza thamani yake.

Mechi zake Bongo:-Ihefu, dk 90, Mtibwa Sugar dk 90, Ruvu Shooting dk 24, Mwadui 71, Kagera Sugar dk 63, Yanga dk 90, Coastal Union dk 45, Polisi Tanzania dk 29, Mbeya City dk 45, KMC dk 45, JKT Tanzania dk 23,Tanzania Prisons dk 45,Mtibwa Sugar dk 30, Mwadui dk 45,Gwambina dk 70,Namungo dk 32.


 

SOMA NA HII  KWA MARA YA KWANZA ..SIMBA WAVUTISHWA PUMZI YA MOTO CHINI YA KOCHA MPYA...WAARABU KAMA KAWA WAMEJIPIGIA..