Home Simba SC MZAWA JOHN BOCCO KUWEKA REKODI YA MABAO

MZAWA JOHN BOCCO KUWEKA REKODI YA MABAO


MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John 
Bocco, amebakisha mabao manne tu, ili kuandika historia mpya ya mabao ya kufunga ndani ya msimu mmoja akiwa na kikosi hicho.

Tangu ametua Simba, idadi kubwa ya mabao ambayo Bocco amewahi kufunga ndani ya msimu mmoja ni 16 aliyoyafunga msimu wa 2018/19, kabla ya hapo, Bocco msimu wa 2017/18 alifunga mabao 14 na msimu uliopita alifunga mabao 9 kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

 Msimu huu tayari ana mabao 13.Mpaka sasa mshambuliaji huyo, ndiye kinara wa mabao ndani ya Simba kwa mabao yake hayo 13, amezidiwa bao moja pekee na kinara Prince Dube kutoka Azam.

 Kuhusu mipango yake Bocco amesema:- “Kama mshambuliaji nina kazi kubwa ya kuhakikisha ninaisaidia timu yangu kufikia malengo tuliyonayo msimu huu.

“Lakini nafurahia kasi niliyonayo, na nimejipanga kutumia kila nafasi nitakayoipata kufunga mabao mengi zaidi.”


SOMA NA HII  SIMBA YAANZA SAFARI KUWAFUATA AL MERRIKH