RASMI leo Julai 20 nyota wa timu ya Ruvu Shooting amemalizana na mabosi wa Azam FC akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake la miezi sita kumeguka ndani ya kikosi hicho.
Awali nyota huyo alikuwa anatajwa kumalizana na Simba ambao waliamua kuwavutia waya mabosi wa Azam FC ili wawaachie beki huyo ila ilielezwa kuwa dili hilo lilibuma.
Kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram wa Azam FC umeandika namna hii:”Tunayofuraha kuingia mkataba wa miaka miwili na beki kisiki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama, kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting.
“Mkataba huo utamfanya Manyama kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023. Manyama ni mmoja wa mabeki wa kushoto wanaoendelea kufanya vizuri kwenye ligi yetu, ingizo lake ndani ya kikosi chetu ni katika kuimarisha zaidi eneo hilo.
“Huo ni usajili wa tatu katika kikosi chetu kuelekea msimu ujao, baada ya awali kuwasaini nyota wa kimataifa wa Zambia, kiungo mshambuliaji, Charles Zulu na mshambuliaji, Rodgers Kola,” .