Home Simba SC KOCHA GOMES YUPO TAYARI KUWAJIBISHWA KWA KUPOTEZA MBELE YA YANGA

KOCHA GOMES YUPO TAYARI KUWAJIBISHWA KWA KUPOTEZA MBELE YA YANGA


 KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, Didier Gomes, bado anaweweseka na kichapo cha bao 1-0 alichokipokea kutoka kwa Yanga.

Kocha Gomes ambaye kabla ya mchezo huo alikua na rekodi ya kukiongoza kikosi chake bila kufungwa mchezo wa Ligi Kuu tangu alipoajiriwa Simba SC mwanzoni mwa mwaka huu, amesema hakutarajia kama angepoteza mbele ya Yanga.

Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa yupo tayari kuwajibishwa kwa namna yoyote ikiwa itahitajika.

“Nipo tayari kuwajibika katika hili kwa nafasi yangu ya ukocha, kwani si jambo zuri kupoteza mechi kubwa ya namna hii ambayo ndani yake ilikuwa na rekodi nyingi bora kama tungepata ushindi.

“Kipindi cha kwanza tulicheza kwa kiwango cha chini jambo ambalo hata upande wangu ilinishangaza licha ya kutenga muda mwingi kuiangalia Yanga namna walivyocheza mechi zao za mwanzo.

“Jambo jingine tulipata nafasi za kufunga wachezaji wangu walishindwa kuzitumia vizuri na kuwafanya wachezaji wa timu pinzani kuendelea kujiamini,” .

Hata hivyo kocha Gomes amesema hana budi kuelekeza nguvu katika michezo ya Ligi Kuu iliosalia, ili kufikia lengo ya kuwapoza machungu mashabiki na wanachama wa Simba SC kwa kutwaa ubingwa wanne mfululizo.

“Tutaweka nguvu kwa ajili ya mechi ya KMC, ili kupata ushindi pamoja na michezo mingine mitatu iliyo mbele yetu dhidi ya Coastal Union, Azam na Namungo ili kuchukua ubingwa kama malengo yetu yalivyo,” .

Ushindi wa juzi Jumamosi (Julai 03) umeiwezesha Yanga kufikisha alama 70, huku ikisaliwa na michezo miwili mkononi kabla ya kumaliza msimu huu 2020/21 baadae mwezi huu.

Simba SC yenye alama 73 inaendelea kubaki kileleni mwa msimamo, huku ikibakiza michezo minne mkononi kabla ya kumaliza msimu huu 2020/21 baadae mwezi huu.


SOMA NA HII  KISA KIWANGO CHA KIBU DENIS...MANULA AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA A-Z ANAYOYAPITIA...