Home Simba SC SIMBA WAKOMAA NA BANDA WA MALAWI

SIMBA WAKOMAA NA BANDA WA MALAWI


KLABU ya Simba inaripotiwa kuwa ‘Siriaz’ na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda anayekipiga kwa mkopo ndani ya klabu ya Sheriff Tiraspol akitokea klabu ya Nyasa Big Bullets.

Simba inataka kumuongeza Banda mwenye umri wa miaka 20, kama mbadala wa Mzimbabwe, Perfect Chikwende ambaye ameonekana kupata wakati mgumu kuendana na utamaduni wa Simba kiasi cha kuondolewa kikosini, huku taarifa zikieleza kuwa huenda Simba ikaachana naye au kumtoa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu.

Hivi karibuni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Zacharia Hanspope alifunga safari na kwenda nchini Malawi, huku ikielezwa kuwa miongoni mwa usajili wa wachezaji ambao alikuwa amekwenda kumalizana nao ni ule wa Banda.

SOMA NA HII  ZILE TETESI ZA 'BEKI KISIKI' NATHAN IDUMBA KUTAKIWA SIMBA ZIMEMUIBUA WAKALA WAKE...KAANIKA UKWELI HUU ..