MSHAMBULIAJI wa Yanga, Wazir Junior amesema kuwa kwake ni jambo zuri kufunga kwa ajili ya timu yake ambapo alifanya hivyo jana Agosti Mosi mbele ya Big Bullets dk ya 8 kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Pia ameweka wazi kwamba kushiriki Kagame ni jambo kubwa hasa ukizingatia ni mashindano makubwa. Msimu huu ameweka wazi kwamba msimu ujao wanaamini watafanya vizuri.