Azam FC

AZAM FC KUIBUKIA MUHIMBILI LEO

admin August 9, 2021 10:44 am


 UONGOZI wa Azam FC uesema kuwa sababu kubwa ya kuweza kupata chano ya Corona ni kuunga juhudi za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu katika mapambano na ugonjwa huo pamoja na kulinda afya zao.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit leo Agosti 9 imeeleza kuwa Azam FC leo watakuwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya chanjo.

“Leo Azam FC tutakuwa Muhimbili kwa ajili ya kupata chanjo ya kujikinga dhidi ya uviko 19, (Corona) ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu katika kupambana na ugonjwa huu kwa kuwa hata yeye amechwanjwa pia.

“Jambo lingine la muhimu ni kulinda afya za wachezaji pamoja na kujilinda kwa kuwa msimu huu Azam FC tutashiriki mashindano ya kimataifa hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari pia,” amesema.

BIASHARA UNITED KUSAJILI WAPYA 9 A-Z KILICHOJIRI UCHAGUZI TFF, TANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply