Home kimataifa CHELSEA YATWAA UEFA SUPER CUP 2021

CHELSEA YATWAA UEFA SUPER CUP 2021

 


CHELSEA ya England ni mabingwa wa UEFA Super Cup baada ya ushindi wa penalti 6-5 dhidi ya Villarreal katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Windsor Park.

Mpaka dakika za nyongeza ngoma ilikuwa Chelsea 1-1 Villarreal. Ni bao la Hakim Ziyech kwa Chelsea inayonolewa  na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel liliwapa nafasi ya kuongoza kwa muda na likawekwa usawa na Gerard Moreno dakika ya 73.

Tuchel anapaswa kujipongeza kwa ajili ya kumfanyia mabadiliko kipa wake Kipa Arrizabalaga ambaye alitoka benchi na kuibuka shujaa baada ya kuchukua nafasi ya Eduardo Mendy katika muda wa nyongeza.

Kepa Arrizabalaga aliweza kuokoa michomo mikali miwili kutoka kwa nyota wa Villarreal inayonolewa na Kocha Mkuu, Unai Emery na kuwafanya Chelsea waweze kutwaa taji lao la pili la Super Cup na likiwa ni la kwanza baada ya kupita miaka 23. Taji lao la kwanza walishinda katika fainali ya 1998 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Madrid.

Tuchel amesema kuwa walijiandaa na walitambua kwamba Kepa ni mzuri katika kuokoa penalti na amebainisha kwamba ana furaha uwepo wa makipa wake wote wawili.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA SIMBA WANYOOSHWA KIMATAIFA KLABU BINGWA NA LEWANDOWSKI