KIPA mpya wa Yanga, Djigui Diarra raia wa Mali kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ametangaza kufiwa na baba yake mzazi.
Katika chapisho aliloweka kwenye ukarasa huo, Diarra ameweka picha yenye maandishi yaliyosomeka ‘Rest in Peace Dad’ na kuelezea kwa maneno kadhaa yaliyoihusisha timu yake mpya ya Yanga.
Diarra ameandika hivi; “Daddy did you dream of seeing me new contract?, You couldn’t wait to see me play at my new club! Daddy I Already ordered a my New Jersey for you Daddy.
Daddy death has separated us but our hearts are bound for eternity,”
Maneno hayo yanaeleza kuwa baba yake Diarra alikuwa anatamani kumuona mwanae akisaini mkataba na timu mpya na alitamani kumuona akiichezea timu hiyo mpya ambayo ni Yanga, na kueleza kuwa tayari alikua amemuagizia baba yake jezi mpya ya Yanga lakini kifo kimewatenganisha japo mioyo yao ipo pamoja.
Diarra ambaye ni kipa wa timu ya taifa ya Mali alisajiliwa na Yanga siku chache zilizopita akitoka katika timu ya Stade Malien ya nchini kwao na bado hajacheza mechi hata moja akiwa ndani ya jezi ya Yanga.