Home Yanga SC SAKATA LA MORRISON NA YANGA NGOMA BADO MBICHI

SAKATA LA MORRISON NA YANGA NGOMA BADO MBICHI


MAHAKAMA ya usuluhishi ya masuala ya kimichezo CAS bado haijaweza kutoa maamuzi yoyote yale kuhusu kesi ya mchezaji wa Simba kwa sasa Bernard Morrison maarufu kama mzee wa kuchetua.


Bado ngoma ni mbichi kwa kuwa muda wowote ule hukumu hiyo inaweza kutolewa.

Kwa mujibu wa CAS kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu siku ya Agosti 24 ila mpaka kufikia majira ya saa sita usiku ngoma ilikuwa haijaeleweka bado.


Klabu ya Yanga ilipeleka shauri lake kwenye mahakama hiyo wakimlalamikia Morrison kuweza kusaini dili jipya ndani a Simba ilihali alikuwa na mkataba wa miaka miwili ndani ya kikosi hicho.


Kwa upande wa mchezaji mwenyewe alikuwa anabainisha kwamba alisaini dili la miezi sita ndani ya Yanga na muda wake uliisha hivyo alisaini dili jipya akiwa ni mchezaji huru.


Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema kuwa nao pia walikuwa wanasubiri majibu kutoka Cas ila hawakuyapata jambo ambalo linawafanya waendelee kusubiri.


“Matarajio yetu ilikuwa ni kuona kwamba tunapata mrejesho wa kesi kwa kuwa hayajatoka basi ni suala la kusubiri kwa kuwa kesi kuna taratibu zake za majibu kutoka,” .

SOMA NA HII  MAFURIKO YA RWANDA YANGA WAFANYA HAYA