Home news HUYU HAPA AKABIDHIWA MIKOBA YA MUANGOLA WA YANGA

HUYU HAPA AKABIDHIWA MIKOBA YA MUANGOLA WA YANGA


 KIUNGO mpya ndani ya kikosi cha Yanga, Jesus Moloko amekabidhiwa rasmi mikoba ya Carlos Carlinhos katika suala zima la kupiga mipira iliyokufa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.


Msimu uliopita Carlinhos raia wa Angola ambaye aliomba kusepa ndani ya kikosi cha Yanga alikuwa na jukumu la kupiga mipira iliyokufa na katika pasi zake tatu ambazo alitoa zote ilikuwa ni kwa mipira ya kona.

Juzi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-1 Rivers United nyota huyo alionekana akipipiga kona nyingi za Yanga jambo linalomaanisha kwamba mikoba ya Carlinhos kapewa nyota huyo.

Yanga ilipata jumla ya kona 7 katika mchezo huo na Moloko aliweza kupiga kona asilimia kubwa ikiwa ni ile ya dakika 37 ambayo ilileta kashikashi kwenye lango la Rivers United.

Licha ya Yanga kuweza kupata kona nyingi ambazo ni 7 huku wapinzani wao wakipiga kona moja walishindwa kutumia mapigo hayo huru jambo ambalo linawaongezea mzigo kuelekea kwenye mchezo wa marudio nchini Nigeria Septemba 18.  

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHEMSHWA NA ISHU YA CHAMA....KIGINGI KINGINE CHA MBRAZILI SIMBA HIKI HAPA...