Home Ligi Kuu MKANDALA ATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA

MKANDALA ATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA


NYOTA wa Dodoma Jiji, Cleophance Mkandala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba ambao utakuwa ni wa mzunguko wa pili.

Dodoma Jiji imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mtupiaji wa bao hilo alikuwa ni Mkandala mwenyewe aliyepachika bao lake la kwanza kwa msimu wa 2021/22 na kuipa pointi tatu muhimu.

Mkandala amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba na kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu,” .

Simba ipo Dodoma imetoka kugawana pointi mojamoja  na Biashara United katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

SOMA NA HII  FT :LIGI KUU BARA-BIASHARA UNITED 0-0 SIMBA