Home Ligi Kuu HII HAPA RATIBA YA LIGI BONGO LEO

HII HAPA RATIBA YA LIGI BONGO LEO


 LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo ikiwa ni mzunguko wa pili kwa timu kuendelea kupambania pointi tatu ndani ya uwanja.

Oktoba 2 viwanja vitatu vitakuwa na kazi ya kuonyesha shughuli ya timu hizo katika kusaka ushindi.

Coastal Union ya Tanga iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC leo inawakaribisha KMC, Uwanja wa Mkwakwani.

KMC imetoka kupokea kichapo mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Karatu, Arusha.

Polisi Tanzania itakutana na Azam FC kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Yanga ambao walitoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya Geita Gold, Uwanja wa Mkapa na itakuwa ni saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  PABLO AANZA KUKIWASHA SIMBA...AJIBU, MKUDE KAMA KAWAIDA YAO...GADIEL MICHAEL MHHH...