Home kimataifa MOURINHO NA ‘SIZITAKI MBICHI HIZI’ KUHUSU KULA SHAVU LA UKOCHA WA NEWCASTLE...

MOURINHO NA ‘SIZITAKI MBICHI HIZI’ KUHUSU KULA SHAVU LA UKOCHA WA NEWCASTLE UNITED


JOSE Mourinho ameondoa uwezekano wa yeye kuwa kocha ajaye wa Newcastle United, lakini anatambua kwamba, “nina uhusiano wenye hisia” na jiji hilo.

Mourinho ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Manchester United, Tottenham Hotspur na sasa AS Roma, hafikirii kurudi tena kwenye Ligi Kuu England.

Baada ya Kampuni ya uwekezaji wa fedha za umma ya Saudi Arabian kuinunua timu hiyo ya St James’ Park, mabadiliko mengi yanatarajiwa katika klabu hiyo.

Steve Bruce amebaki kuwa kocha mkuu kwa sasa, lakini uvumi umezagaa kuhusu hatima yake, huku wamiliki wapya wakiwa wanataka kocha mwenye rekodi kubwa.

Mourinho anaweza kufiti kwenye nafasi hiyo hasa kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye ligi za Ulaya pamoja na mashindano makubwa ya bara hilo.

Lakini alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuhamia Newcastle, Mourinho amesema uwezekano huo kwa sasa haupo kwani ana mkataba na Roma, ambayo inamilikiwa na bilionea wa Marekani, Dan Friedkin.

Mourinho alihamia kwa klabu hiyo yenye maskani yake mji mkuu wa Italia, baada ya kutangazwa kuteuliwa Mei mwaka huu.

Amesema anahisia nzuri sana na jiji la Newcastle kwani ni sehemu anayoipenda, pia alikuwa na ushirikiano mzuri na Robby Robson wakati akiifundisha Barcelona ambayo baadaye alikwenda kuinoa timu hiyo ya Magpies.

“Kitu pekee ninachoweza kusema ni kwamba, kwa miaka mingi, mingi sana, nilifanya kazi na mtu ambaye ni muhimu zaidi katika historia ya Newcastle, Sir Bobby Robson,” alisema Mourinho.

“Na kwa sababu ya hilo nimekuwa na uhusiano wenye hisia ya aina yake na jiji lile na mashabiki wake.”

SOMA NA HII  NI VIKOSI GHALI KINOMA ULAYA