Home kimataifa RONALDO AMPIKU MESSI KWENYE SUALA LA HATTRICK

RONALDO AMPIKU MESSI KWENYE SUALA LA HATTRICK


 WABABE wawili kwenye ulimwengu wa soka bado wanakimbizana kwenye ishu ya kuandika rekodi ambapo kila mmoja anazidi kupambana kuweka mambo sawa.

Ukitaja wachezaji wawili ambao wanatawala soka la dunia kwa zama za sasa ikiwa ni katika kipindi cha miaka 12 huwezi kuacha kumtaja Cristiano Ronaldo raia wa Ureno na Lionel Messi mwamba raia wa Argentina.

Wachezaji hawa wameweza kuchukua Ballon d’or 11 wote wawili idadi kubwa kwao ambapo katika hili mbabe alikuwa ni Messi ambaye amechukua tuzo hiyo kubwa mara 6 na Cristiano akichukua mara 5.

Katika kipindi ambacho Messi aliweza kusepa na tuzo hiyo ya Ballon d’0r  alikuwa ndani ya Klabu ya Barcelona  na Cristiano yeye amepata mafanikio akiwa anatumika klabu tofautitofauti ikiwa ni pamoja na Manchester United, Juventus na Real Madrid.

Kwenye kitengo cha kufunga  Hatrick hapa Ronaldo kampoteza mazima Messi ambapo jumla Ronaldo amefunga hat trick 58 huku mshikaji wake Messi akiwa na hat trick 55.

Toafuti yao hapa ni tatu pekee lakini kwenye rekodi ni jambo kubwa na inamfanya CR 7 kuwa mbabe katika hili kama ambavyo kwenye Ballon d’Or tofauti yao ikiwa ni namba moja pekee.

Messi amefunga Hatrick 48 kwa ngazi ya klabu na 7 akiwa na timu ya Taifa ya Argentina wakati Cristiano amefunga hatrick 48 kwa ngazi ya klabu na 10 akiwa na timu ya Taifa ya Ureno.

Katika hatrick hizo inaonesha kuwa asilimia 50 sawa na hatrick 31 Cristiano Ronaldo amefunga kwa mikwaju ya penati na Messi ikiwa ni asilimia 25 sawa na penati 14.

Nyota hawa wawili wote ni washakji na majina yao pia yameorodheshwa kwenye orodha ya wale wanaowania tuzo ya Ballon d’0r ya mwaka huu.

Pia wakiwa kwenye majukumu yao ya timu zao za taifa wanavaa vile vitambaa vya unahodha, acha kazi iendelee.


SOMA NA HII  BILIONEA WA LIVERPOOL AJITOKEZA KUTAKA KUINUNUA CHELSEA...MATAJIRI WENGINE HAWA HAPA...