SIMBA muda wowote watakamilisha usajili wa beki wa kati wa Biashara United, Abdoulmajid Mangalo katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, mwaka jana.
Beki huyo alikuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo pamoja na Abdoultwalib Mshery na Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na Denis Nkane ambao tayari wametambulishwa.
Simba hivi sasa ipo katika mipango ya kuachana na beki wake wa kati Muivory Coast, Pascal Serge Wawa ambaye nafasi yake huenda akaichukua Mangalo.
Taarifa ambazo imezipata na kuziripoti gazeti la Championi Jumatatu, mabosi wa Simba wamevutiwa na kiwango bora ambacho Mangalo amekionyesha katika misimu miwili mfululizo.
Aliongeza kuwa sababu ya kwanza ya kumsajili ni uzoefu na uwezo mkubwa wa kucheza michuano ya kimataifa ambaye akiwa na Biashara United walicheza Kombe la Shirikisho Afrika katika msimu huu.
“Asilimia 60 Simba wamemalizana na Mangalo na anachosubiria ni kusaini na kutambulishwa mara baada ya taratibu zote za usajili kukamilika.
“Tayari Simba wamewafuata Biashara kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kukamilisha dili hilo la usajili katika dirisha dogo,” alisema mtoa taarifa huyo.
Akizungumzia usajili Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema kuwa: “Tupo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao hivi sasa ni siri kuwaweka wazi hadi pale taratibu zote za usajili zitakapokamilika.