Home news MORRISON BANA…PAMOJA NA KUWA NA VITUKO VINGI VYA KUKERA…KUMBE ‘SOMETIME YES’…

MORRISON BANA…PAMOJA NA KUWA NA VITUKO VINGI VYA KUKERA…KUMBE ‘SOMETIME YES’…


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison, amefunguka kwamba, kwa sasa anajipanga kuhakikisha anaisaidia timu yake kushinda mechi ya nusu fainali na kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Kauli ya Morrison imekuja baada ya Simba kumaliza kinara wa Kundi C ikikusanya pointi nne katika michuano hiyo inayoendelea Zanzibar na kutinga nusu fainali ikitarajiwa kucheza na Namungo, leo Jumatatu.

Katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliochezwa juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan, Simba ilishindwa kufungana na Mlandege.

Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison amesema kuwa: “Mlandege ni timu nzuri, hii sio mechi yetu ya kwanza kukutana, huko nyuma tushawahi kucheza nao, ni timu yenye ushindani mkubwa sana.

“Tulijitahidi kuhakikisha tunapata ushindi, lakini tumeukosa. Kwa sasa tunaangalia hatua inayofuata ya nusu fainali ambayo tutahakikisha tunashinda na kuingia fainali kwenda kuchukua ubingwa.”

SOMA NA HII  SIMBA YATAMBA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA