Home news PAMOJA NA KUONYESHA KIWANGO KIKUBWA…SAIDO MBIONI KUIKIMBIA YANGA…ISHU YA MKATABA YATAJWA…

PAMOJA NA KUONYESHA KIWANGO KIKUBWA…SAIDO MBIONI KUIKIMBIA YANGA…ISHU YA MKATABA YATAJWA…

 


IMEFAHAMIKA kuwa nyota Mrundi wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, yupo njiani kuondoka ndani ya kikosi hichobaada ya kupata ofa kadhaa nje ya nchi ikiwemo klabu za Afrika na Uarabuni.

Nyota huyu ambaye anamaliza mkataba wake na Yanga msimu huu, amekuwa tegemeo kwenye kikosi hicho hasa linapokuja suala la mipira iliyokufa.

Mtu wa karibu na nyota huyo, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Mkataba wa Saido na Yanga unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na mpaka sasa ana ofa nyingi nje ya Tanzania zikiwemo ndani ya Afrika na Uarabuni.

“Kama Yanga wakiendelea kukaa kimya, basi tunaweza kumuona mchezaji akiondoka hata kipindi hiki cha dirisha dogo au akasubiri hadi mkataba wake ukimalizika.”

Alipotafutwa Saido kuzungumzia hilo, alisema: “Kwa sasa si wakati sahihi kuzungumzia masuala hayo.”

SOMA NA HII  MUDA WA HESABU KWA SASA, MUHIMU KUJIPANGA