Home Habari za michezo PETER BANDA AZIDI KUNG’ARA SIMBA…AWAPIGA MWELKEA WA KARNE KINA KAPOMBE…

PETER BANDA AZIDI KUNG’ARA SIMBA…AWAPIGA MWELKEA WA KARNE KINA KAPOMBE…


Winga wa Simba, Peter Banda amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Banda amewapiku kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ambao aliingia nao fainali.

Katika mwezi Machi Banda amecheza mechi nne sawa na dakika 226 akionesha kiwango safi na kusaidia kupatikana kwa bao moja (assist).

Mchanganuo wa kura ulikuwa kama ifuatavyo;

  1. Banda Kura 2682, sawa na asilimia 74.
  2. Sakho kura 744 sawa na 20.
  3. Kapombe Kura 218 sawa na asilimia 6.
SOMA NA HII  CEO WA SIMBA AANZA NA HILI KIMATAIFA...