Home Habari za michezo BAADA YA KUONA TUMEPANGWA NA ALGERIA NA UGANDA..KIM POULSEN KAGUNA KISHA AKASEMA...

BAADA YA KUONA TUMEPANGWA NA ALGERIA NA UGANDA..KIM POULSEN KAGUNA KISHA AKASEMA HAYA…


Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa STars’ Kim Poulsen amewataka Watanzania kuwa na imani na timu yao, licha ya kuangukia kwenye kundi lenye vigogo wa Afrika Algeria.

Taifa Stars juzi Jumanne (April 20) ilipangwa Kundi F lenye timu za Algeria, Uganda na Niger katika safari yake ya kusaka nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zitakazounguruma Ivory Coast.

Kocha Kim amesema Watanzania wengi huenda wamepata mshtuko baada ya kuona Taifa Stars imeangulia kwenye kundi hilo, lakini kwake anaamini timu yake ina nafasi ya kupambana na kufanya vizuri.

Amesema kanuni za kufuzu fainali za AFCON zinatoa nafasi kwa timu mbili kwa kila kundi, hivyo hadi sasa Tanzania ni sehemu ya timu ambazo zina uwezo wa kupata nafasi moja kati ya hizo kupitia Kundi F.

“Nafikiri Makundi yote walio juu kwa viwango wanapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi moja ya kufuzu, lakini kwangu ni tofauti kwa sababu kundi bado lipo wazi na yoyote anaweza kupita ikiwemo Tanzania.”

“Kila timu inapaswa kupambana ili kuwa sehemu ya timu mbili zitakazofuzu, kwa Taifa Stars tutajiandaa kikamilifu ili tufanikiwe kupata alama ambazo zitatuvusha na kufuzu AFCON 2023.”

“Ninaowamba Watanzania waendelee kuwa na Taifa Stars, waiamini timu yao na waipende wakati wote itakapokua kwenye mchakato wa kusaka nafasi ya kushiriki AFCON 2023, ikiwa hivi ninaimani tutafanikiwa.” amesema Kocha huyo kutoka Denmark.

Mara ya mwisho Taifa Stars ilifuzu Fainali za AFCON mwaka 2019 zilizounguruma nchini Misri, na kutolewa hatua ya makundi.

SOMA NA HII  AMBANGILE:- YANGA WAKIJISAHAU NA HILI WATAPIGWA GOLI ZA KUTOSHA NA MAMELOD....