Home Habari za michezo SPOTIFY WAIKOA BARCELONA NA NJAA YA PESA ….WAKUBALI KUBADILI JINA LA UWANJA...

SPOTIFY WAIKOA BARCELONA NA NJAA YA PESA ….WAKUBALI KUBADILI JINA LA UWANJA WAO CAMP NOU…


Mkataba wa kihistoria wa udhamini wa Barcelona na Spotify ni “moja ya dili bora zaidi duniani” alisema Makamu wa rais Juli Guiu baada ya kupewa baraka zote siku ya Jumapili.

Katika mkutano wa Barca ilipigwa kura ya asilimia 89 ya kuunga mkono makubaliano yenye faida kubwa na kampuni hiyo kubwa ya utiririshaji wa sauti za muziki.

Miamba hao wa Catalan wameuza haki za majina ya Camp Nou kwa miaka 12 ijayo – minne kati ya hiyo itatumika kufanya ukarabati wa uwanja na minane baada ya kazi kukamilika.

Mojawapo ya kumbi maarufu zaidi za michezo ulimwenguni itajulikana kama Spotify Camp Nou, wakati jina la kampuni ya Uswisi litaonekana mbele ya mashati ya timu ya wanaume na wanawake, kuanzia 2022-23 na kwa misimu minne ifuatayo.

Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kuwa dili hilo litaipatia Barca zaidi ya Euro milioni 400, ikiwa ni sindano inayohitajika sana ya fedha kwa klabu ambayo imeingia kwenye matatizo makubwa ya kifedha.

Guiu alisema: “Ni makubaliano bora zaidi ya udhamini katika historia ya jezi ya Barcelona.”

“Ni makubaliano ya kihistoria kwa sababu ni makubaliano bora zaidi ya udhamini kwa Barca na ni ushirikiano wa kimkakati kati ya Barca na Spotify,”

SOMA NA HII  MIEZI KADHAA TOKA ASEPE...ZORAN MAKI AANIKA A-Z KILICHOMKIMBIZA SIMBA HARAKA....