Home Uncategorized AZAM FC YAKWAMA MBELE YA KMC UHURU

AZAM FC YAKWAMA MBELE YA KMC UHURU


 JUMA Kaseja, nahodha wa Klabu ya  KMC leo Novemba 21 ameongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Azam FC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 imepoteza mchezo wake wa pili leo na ule wa kwanza ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo ilifungwa pia bao 1-0 na kufanya ipoteza pointi sita kwa kufungwa huku ikiwa imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Bao pekee la KMC lilifungwa na Relliats Lusajo mshambuliaji wa zamani wa Namungo dakika ya 57 na kufanya Azam FC wakwamwe kwa mara ya kwanza wakiwa Dar kwa kuwa ule mchezo wa kwanza walipoteza wakiwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Wakati Azam FC ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru,JKT Tanzania ikiwa nyumbani, Uwanja wa Jamhuri Dodoma imefungwa mabao 2-0 dhidi ya Gwambina.


Mabao ya Gwambina yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 84 likiwa ni bao lake la kwanza ndani ya ligi kwa msimu huu wa 2020/21 na Meshack Abraham dakika ya 72 ambaye anafikisha bao lake la tano.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YATUMA UJUMBE HUU KWA KMC