Kocha wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma na mchezaji wa timu hiyo Jamali Mtegeta wamefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh 500,000 kila mmoja kwa kosa la kushambuliana kwa mateke wakati mchezo dhidi ya Biashara United ukiendelea kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.
Kocha Masoud Djuma alimpiga teke mchezaji Jamali Mtegeta aliyekuwa kwenye benchi kabla mchezaji huyo hajarejesha pigo la aina hiyo kwa kocha wake.
Masoud Djuma ambaye amerudi Tanzania kw amara ya pili na kufanikiwa kupata ajira kwenye timu hiyo, bado hajaweza kuwa na matokeo ya muendelezo wa ushindi tangia alipopata kibarua cha kuifundisha timu hiyo.