Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SIMBA LEO…MKWASA KAJIPIGA PIGA KIFUANI NA KUTOA KAULI HII...

KUELEKEA MECHI NA SIMBA LEO…MKWASA KAJIPIGA PIGA KIFUANI NA KUTOA KAULI HII YA KIBABE AISEE…


KOCHA wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akiwaambia wasiogope, kwani anaamini nidhamu itawapa pointi tatu leo dhidi ya Simba wa Ligi Kuu Bara.

Mkwasa alisema mchezo uliopita na Yanga ulioisha kwa suluhu uliwapa morali wachezaji na leo watashuka ili kukamilisha jambo lao katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tunaenda katika mchezo huu kwa tahadhari kubwa kama tulivyocheza na Yanga, ni mechi ngumu hivyo ili kupata kile tunachokikusudia yatupaswa kujiandaa kimwili na kiakili,” alisema.

Hii ni mara ya tatu kwa timu hizo kukutana msimu huu baada ya awali Ruvu kufungwa 3-1 na Simba katika mechi ya kwanza wa Ligi uliopigwa jijini Mwanza kisha kuchapwa mabao 7-0 katika ASFC raundi ya 16 Bora, Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI....AZAM FC WAAMUA KUIFANYIA 'MAJAMBOZI' YA UHAKIKA YANGA SC...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here