Home Habari za michezo AL AHLY WAIIGA SIMBA ….NOA WAMPA ULAJI KOCHA KUTOKA URENO…WATAMLIPA ZAIDI YA...

AL AHLY WAIIGA SIMBA ….NOA WAMPA ULAJI KOCHA KUTOKA URENO…WATAMLIPA ZAIDI YA BILIONI TATU ZA KIBONGO…


Kocha José Ricardo Ribeiro Soares mwenye umri wa miaka 47, amewasili Cairo nchini Misri kwa ajili kuanza kazi rasmi ya kuwanoa miamba wa Soka Barani Afrika, Al Ahly kama Kocha wao Mkuu.

Soares ambaye ni raia wa Ureno anachukua mikoba ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Pitso Misomane raia wa Afrika Kusini ambaye alifungashiwa virago hivi karibuni na tayari ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo Kabla ya kutua Al Ahly, Soares alikuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Gil Vicente ya nchini kwao Ureno.

Pia amewahi kufundisha timu mbalimbali tangu alipoanza kazi ya ukocha mwaka 2005 ikiwemo;


  1. Moreirense FC: 19/20 (Dec 18, 2019) – 20/21 (Nov 9, 2020)
  2. SC Covilhã: 19/20 (Jul 1, 2019) – 19/20 (Dec 17, 2019)
  3. Académica Coimbra: 17/18 (Nov 14, 2017) – 17/18 (Apr 1, 2018)
  4. Desportivo Aves: 17/18 (Jul 1, 2017) – 17/18 (Oct 2, 2017)
  5. GD Chaves: 16/17 (Dec 20, 2016) – 16/17 (Jun 30, 2017)
  6. FC Vizela: 14/15 (Jan 7, 2015) – 16/17 (Dec 19, 2016)
  7. FC Felgueiras: 1932 – 14/15 (Jul 1, 2014) – 14/15 (Jan 6, 2015)
  8. GD Ribeirão: 13/14 (Aug 27, 2013) – 13/14 (Oct 14, 2013) CA
  9. Felgueiras: 11/12 (Jul 1, 2011) – 12/13 (Jun 30, 2013)
  10. FC Lixa Lixa: 09/10 (Jul 1, 2009) – 10/11 (Jun 30, 2011)
  11. GDU Torcatense: 06/07 (Mar 26, 2007) – 06/07 (Jun 30, 2007)
  12. Caçadores das Taipas: 05/06 (Jul 1, 2005) – 06/07 (Jan 15, 2007).

Soares amevunja mkataba wake na na Gil Vicente kwa kuwalipa pauni 250,000. Katika makubaliano yake na Alhy atasaini kandarasi ya miaka miwilili ambapo katika kandarasi hiyo atakusanya pauni milioni 1.5 kwa mwaka ambayo ni sawa na zaidi ya Bilioni tatu za kitanzania.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA...HAWA HAPA MAREFA WA MCHEZO HUO