Home Habar za Usajili Simba ISHU YA MOSES PHIRI NA SIMBA…? UKWELI WOTE HUU HAPA…HAKUNA JIPYA NI...

ISHU YA MOSES PHIRI NA SIMBA…? UKWELI WOTE HUU HAPA…HAKUNA JIPYA NI YALE YALE..

 


Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Moses Phiri (27) amejiunga na miamba hiyo ya Msimbazi.

Nyota huyo wa Klabu ya Zanaco ya Zambia amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Simba SC na anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Phiri ambaye alikuwa mfungaji Bora wa ligi kuu ya Zambia msimu wa 2020/2021 akiwa na magoli 13.

Inaelezwa kuwa, Phiri anakwenda kuchukua nafasi ya Mkongomani, Chris Mushimba Mugalu (31) ambaye anadaiwa Simba itaachana naye kutokana kiwango chake kutoridhisha msimu huu unaomaliza.

Habari za Phiri kusajiliwa na Simba si geni, kwani ilifaamika kitambo kuwa nyota huyo angetua msimbazi kutokana na kuwa alishasaini mkataba wa awali, kitu ambacho kiliinyong’onyeza Yanga na kuamua kuachana naye.

Mchezaji huyo atakumbukwa na wengi mara baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa kirafiki na Yanga, kwenye kilele cha siku ya wananchi mwanzoni mwa msimu huu.

Wachezaji wanaowindwa na Simba mpaka sasa 1. Ceasar Manzoki – Straika 2. George Mpole – Straika 3. Morlaye Sylla – Kiungo 

DONE DEAL 

1. Moses Phiri – Straika.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI YA KARIAKOO...HITIMANA ASHINDWA KUJIZUIA SIMBA..AFUNGUKA KUHUSU PRESHA YAO...